.

Wednesday, July 20, 2016

Watengenezaji wa meli wamesema hii ndio meli kubwa zaidi duniani itakayokuwa ikibeba abiria. Meli hii imepewa jina la Harmony of the Seas. Inawafanya kazi 3,000,inauwezo wa kuchukua abiria 6780,  kwa wiki kutembea na hii meli ni £900 kwa mtu mmoja, ila kwenye eneo la bata ni £2,760 kwa mtu mmoja.
Watengenezaji wa meli hii wanasema imechukua miezi 32 kujenga meli hii ya Harmony of the Seas, ni meli ya 25 kwenye meli za Royal Caribbean International fleet.

Tuesday, November 24, 2015

WANANCHI WA KIYOGO WAKIWA KATIKA MKUTANO NA VIONGOZI WAO KATIKA KUPANGA KAZI ZA KIMAENDELEO IKIWEMO NA UJENZI WA SHULE YA MSINGI YENYE UBORA
NYUMBA YA MGANGA ILIYOJENGWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA KIYOGO IKIWA HAINA MFANYAKAZI
ZAHANATI ILIYOJENGWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA KIYOGO KWA NGUVU ZAO NA KUAHIDIWA NA MKUU WA WILAYA YA LUDEWA BW.JUMA MADAHA KUWA ATAWALETEA MFANYAKAZI WAKIKAMILISHA UJENZI WA VYOO
WANAKIJIJI CHA KIYOGO WAKIFANYA KAZI ZA MAENDELEO KWA KUJENGA VYOO VYA ZAHANATI NA MGANGA ATAKAYEPELEKWA KUFANYA KAZI KATIKA KIJIJI HICHO
WANAFUNZI WA KIYOGO WAKIWA KATIKA DARASA LAO LILILOPANGWA TOFARI TOKEA SHULE HIYO IANZISHWE NI ZAIDI YA MIAKA 10 HAIJAKARABATIWA ZAIDI YA NGUVU ZA WANANCHI NA MSAADA WA BATI KUTOKA SHIRIKA LA CONSEIN
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KIYOGO WAKIWA DARASANI NA MWALIMU WAO KATIKA DARASA AMBALO HALIJAWAHI SAKAFIWA
SHULE YA MSINGI KIYOGO IKIWA KATIKA HALI MBAYA TANGIA IJENGWE HAIJAWAHI FANYIWA UKARABATI NI ZAIDI YA MIAKA MITANO
MAJI YA MTO RUHUHU YANAYOTUMIWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA KIYOGO KWA KUNYWA NA MATUMIZI MENGINE YAKIWA YAMECHAFULIWA NA WACHIMBA MADINI

Saturday, July 25, 2015

9
Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita

utendaji wake.

 Baadhi ya wazee wa wilaya ya Ludewa wakimpa baraka za mwisho za kuanza kugombea kwa awamu ya pili Mh.Deo Filikunjombe
Filikunjombe akisikiliza nasaha za Wazee

 msafara wa kumsikindikiza kutangaza nia ya kugombea ubunge Deo Filikunjombe ukiingia viwanja vya mpira wa miguu Ludewa mjini
Filikunjombe akiwasalimia mamia ya wanachama wa ccm wilayani Ludewa ambao walikuja kumuunga mkono

wasanii wa kikundi cha IVA YOUTH GROUP ambacho ni kikundi cha uhamasishaji wilayani hapa wakifanya yaliyo yao
mamia ya washabiki wa ccm wakimraki Filikunjombe

Filikunjombe akiongea na wananchi wa wilaya ya Ludewa kata ya Ludewa mjini wakati akitangaza nia ya kugombea ubunge

msanii wa IVA youth Group Seleman Chikuti akionesha umahiri wake katika sanaa

Sunday, July 5, 2015

MGAWANYO WA TANZU NA VIPERA VYA FASIHI SIMULIZI.

 M.M Mulokozi(1989)

Katika makala hii tunaanza na kuelezea maana ya fasihi, fasihi fasihi simulizi kwa kutumia wataalam mbalimbali, baada ya kuelewa vizuri dhana hizi tutajadili vigezo vilivyotumika katika mgawanyo wa tanzu na vipera vya fasihi simulizi katika makala ya M.M Mulokozi (1989) na hatimaye tutaangalia ubora na udhaifu wa uainishaji wa tanzu hizo, na kumalizia na hitimisho, kielelezo na mwisho marejeo.
Fasihi ni sanaa itumiayo lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii bila kujali kuwa imeandikwa au haijaandikwa. Fasihi ambayo haijaandikwa ni fasihi simulizi na fasihi iliyoandikwa ni fasihi andishi.
Ama kuhusu Fasihi simulizi, Wamitila ( 2002) anaeleza kuwa Fasihi simulizi ni fasihi ambayo huwasilishwa kwa njia ya mdomo kwa kusimuliwa, kuimbwa , kutongolewa au kughanwa.
Naye Mulokozi (1996) anaelezea kuwa fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya mdomo na vitendo bila maandalizi.
Kwa ujumla fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya masimulizi  ya mdomo na vitendo bila maandishi.
Katika makala ya M.M Mlokozi (1989) katika mulika ya 21 amejaribu kuzigawa tanzu za fasihi simulizi ya Tanzania katika tanzu zake mahususi kwa kuzingatia VIGEZO vifuatavyo;
Umbile na tabia ya kazi inayohusika;upande wa umbile na tabia ya kazi ya sanaa ameangalia vipengele vya ndani vinavyoiumba sanaa na kuipa mwelekeo au mwenendo ilionao.Vipengele hivyo ni namna lugha inavyotumika(kishairi,kinathali,kimafumbo,kiwimbo, kighani nakadharika) pia muundo wa fani hiyo na wahusika kama wapo.
Kigezo cha pili ni muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira (hili linazingatia pia dhima yake kijamii) hapa Mulokozi amezingatia ukweli wa msingi kuwa fasihi simulizi ni sanaa inayo pita, isiyofungwa katika umbo maalum, wala matini maalum yasiyo badilika. Fasihi simulizi inatawaliwa na vitu muhimu vitatu yaani watu, wakati na mahali. Mwingiliano huu ndio muktadha, na muktadha ndio unaamua fani fulani ya fasihi simulizi ichukue umbo lipi? Iwasilishe vipi kwa hadhira, kwenye wakati na mahali hapo.

Zifuatazo ni tanzu na vipera vya fasihi simulizi kama zilivyoainishwa na M.M.Mlokozi(1989) katika mulika 21 na jinsi alivyo ziainisha kwa kutumia vigezo hivi viwili, yaani kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishwaji kwa hadhira, na vipera vyake.
M.M.Mulokozi ameainisha tanzu sita ambazo ni; mazungumzo, masimulizi, maigizo (drama) ushairi semi na ngomezi (ngoma). Hivyo ufuatao ni uainishaji wa tanzu hizi za fasihi simulizi na vipera vyake kwa kutumia vigezo vya Mulokozi katika mulika ya 21.
Mazungumzo, ni maongezi au maelezo ya mdomo katika lugha ya kawaida, juu ya jambo lolote lile. Si kila mazungumzo ni fasihi mazungumzo ili yawe fasihi lazima yawe na usanii wa aina fulani, na uhalisia baada ya kuunakili.
Tanzu zinazoingia katika fungu la mazungumzo; Hotuba, Malumbano ya watani, Ulumbu, Soga na mawaidha. Katika kuainisha tanzu hizi ndani ya mazungumzo M.M.  Mulokozi ametumia vigezo vyote viwili; Hotuba, malumbano ya watani, ulumbu, soga na mawaidha. Kwa kuzingatia kigezo cha kwanza kinachozingatia msingi wa umbile na kazi inayohusika, tunaona tanzu hizi zote zina vipengele vya vinvyoumba sanaa na kuipa muelekeo au mwenendo ulionao, katika hotuba, malumbano ya watani, ulumbu, soga na mawaidha vyote vinavipegele vyake. Pia tanzu hizo zote zina maana ya lugha inayotumika. Mfano katika hotuba lugha rasmi ndiyo inayotumika, katika malumbano ya watani lugha ya kejeli mara nyingi ndio hutumika zaidi, mawaidha hutumia lugha rasmi au lugha za kikabila hutumika.
Pia katika kigezo umbile na tabia ya kazi inayohusika,katika kuainisha tanzu hizi mulokozi ametumia muundo wa fani na wahusika kama wapo.Tanzu zote hizo katika mazungumzo zina fani yake. Mfano katika malumbano ya watani ni tanzu inayozingatia fani zifuatazo; Kuna utani wa mababu, mabibi na wajukuu, utani wa mashemeji, utani wa kikabila na utanu wa marafiki. Kila kimojawapo kati ya fani hazi huwa na kanuni zake, miktadha yake na mipaka yake katika jamii zinazohusika.
Pia katika kuanisha tanzu za mazungumzo Mulokozi ametumia kigezo chake cha pili yaani kigezo kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira hili linazingatia pia dhima yake katika jamii kama ifuatavyo;

Ndani ya mazungumzo kuna hotuba, mawaidha, ulumbu, malumbano ya watani, soga; Tanzu hizi zote zinazingatia msingi wa fasihi kuwa ni sanaa inayopita, isiyofungiwa katika umbo maalum, wala matini yasiyobadilika. Mfano Hotuba ni sanaa inayopita, isiyofungwa katika umbo maaluma na matini yake hubadilika kulingana na matukio kama vile; matukio ya kidini, sherehe na kadharika. Hotuba hufuata wakati, watu na mahali. Katika kigezo hiki kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira huzingatia wakati, watu na mahali.Tunaona katika mazungumzo na tanzu zake zinazingatia wakati watu na mahali, mfano mawaidha huzingatia watu gani,wana umri gani, je ni vijana wa kiume au wa kike. Pia huzingatia mahali yaani tukio linapofanyika, mfano sebuleani au chumbani na pia wakati gani asubuhi, mchana au jioni.
Tanzu ya mazungumzo kwa ujumla imeainishwa kwa kutumia vigezo vyote viwili yaani kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira.
Masimulizi; ni fasihi yenye kusimulia habari  fulani.  Mulokozi (1989) anasema kuwa masimulizi ni fasihi ya kihadithi na fani zake huwa na sifa zifuatazo; hueleza atukio katika mpangilio fulani mahsusi, huwa na wahusika yaani watendaji au watendwaji katika matukio yanayosimulia, hutumia lugha ya kimaelezo, utambaji wake au utoaji wake huweza kuambatana na vitendo au ishara, na huwa na maudhui ya kweli au ya kubuni na yenye mafunzo fulani katika jamii.

Sunday, June 28, 2015

RAIS KIKWETE AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI WA NGAZI YA JUU KWA MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA LEO UKONGA, JIJINI DAR

9
Rais Kikwete akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja  ithabati rasmi kwa ajili ya Chuo cha Mafunzo cha Ukonga iliyotolewa na  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga.  11
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akimvisha Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Megereza,  Amina Juma Lidenge kwa niaba ya wahitimu wenzake 104  wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam.12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku cheo Mwanafunzi Alyefanya Vizuri Katika Masomo ya darasani Inspekta Saidi Jacob Seni  wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam.
10
Askari Magereza wa enzi za Mkoloni wakionesha ukakamavu wao mbele ya Rais Kikwete  wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam.
7
Rais Jakaya Mrisho kikwete akifunga  Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015. PICHA ZOTE NA IKULU

2
Rais Jakaya Mrisho kikwete akisalimiana na maafisa wanaoshughulikia kitengo cha SACCOS cha Magereza kwenye banda la maonesho ya sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015.
   8
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe akipogea ithabati rasmi kwa ajili ya Chuo cha Mafunzo cha Ukonga kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga.
13
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la wahitimu  104  wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015
14
3
Rais Jakaya Mrisho kikwete na  Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja  wakifurahia samani katika  banda la maonesho ya sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga.
4
Rais Jakaya Mrisho kikwete  na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja  wakiwa na Wakuu wa Jeshi la Magereza wa nchi za SADC na Kenya waliohudhuria  sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015
1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja  wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Wakuu wa Magereza Wastaafu. Kutoka kulia ni Mhe. Augustine Nanyaro, Mhe. Nicas Pius Banzi, Kamishna Generali Mkuu wa sasa John Minja, Rais Kikwete, Alhaj Jumanne Mangara, Mzee John Mwanguku, na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji Mstaafu Mama Aziza Mursali sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015.
5
6
Rais Jakaya Mrisho kikwete na  Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja  wakiwa na wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015
9
Rais Kikwete akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja  ithabati rasmi kwa ajili ya Chuo cha Mafunzo cha Ukonga iliyotolewa na  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga.  11
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akimvisha Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Megereza,  Amina Juma Lidenge kwa niaba ya wahitimu wenzake 104  wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam.12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku cheo Mwanafunzi Alyefanya Vizuri Katika Masomo ya darasani Inspekta Saidi Jacob Seni  wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam.
10
Askari Magereza wa enzi za Mkoloni wakionesha ukakamavu wao mbele ya Rais Kikwete  wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam.
7
Rais Jakaya Mrisho kikwete akifunga  Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015. PICHA ZOTE NA IKULU

2
Rais Jakaya Mrisho kikwete akisalimiana na maafisa wanaoshughulikia kitengo cha SACCOS cha Magereza kwenye banda la maonesho ya sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015.
   8
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe akipogea ithabati rasmi kwa ajili ya Chuo cha Mafunzo cha Ukonga kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga.
13
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la wahitimu  104  wakati wa sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015
14
3
Rais Jakaya Mrisho kikwete na  Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja  wakifurahia samani katika  banda la maonesho ya sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga.
4
Rais Jakaya Mrisho kikwete  na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja  wakiwa na Wakuu wa Jeshi la Magereza wa nchi za SADC na Kenya waliohudhuria  sherehe za Kufunga Mafunzo ya Uongozi ya Ngazi za Juu Kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo Cha Maafisa wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2015

Tuesday, June 23, 2015

Joto kali 

Waziri mkuu nchini Pakistan Nawaz Sharrif ametaka hatua za dharura kuchukuliwa huku idadi ya watu waliofariki kutokana na wimbi la joto katika mkoa wa kusini wa Sindh ikifikia 700.
Mamlaka ya kukabiliana na majanga ya dharura NDMA imesema kuwa imepokea maagizo kutoka kwa
Nawaz Sharrif kuchukua hatua za dharura.
null
 Joto kali 
Jeshi tayari limepelekwa katika eneo hilo kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili kuisaidia mamlaka hiyo.
Wengi wa waathiriwa ni watu wazima kutoka kwa familia zinazopata mapato ya chini.
null
 Joto kali 
Maafisa wa afya wanasema vifo vingi vimetokea katika mji mkuu wa Karachi ambao ulikumbwa na joto la viwango vya juu vya hadi digree 45 c.
Katibu wa afya katika mkoa wa Sindh Saeed Mangnejo amesema kuwa watu 612 walifariki katika hospitali kuu ya serikali mji huo katika kipindi cha siku nne zilizopita.
null
 Joto kali
Wengine 80 wameripotiwa kufariki katika hospitali za kibinafsi.null

Categories

Popular Posts